Simon Kitururu - Nafasi ya katibu.

Tuesday 15 May 2007

WASIFU:
Umri: Miaka 33.
Utaalamu: Mtaalamu wa biashara.

Kwa nini anagombea kuwa katibu:-

Nagombea nafasi ya Ukatibu nikiwa na dhumuni la kuimarisha jumuiyakatika kipindi hiki cha mwanzo.Ikiwa ni pamoja nakuhakikisha jumuiya inakuwa na katiba na kamati zifanyazo kazi. Najua mwanzo ni mgumu na ninaamini nina uwezo wakukabiliana na ujenzi wa jumuiya hii hasa kipindi hiki cha mwanzo cha ujenzi wa msingi imara wa jumuiya.

http://www.simon-kitururu.blogspot.com/

http://www.fikira.blogspot.com/

Naombeni kura zenu.
 
© Blogu Tanzania | Tarehe: 5/15/2007 |

Maoni: 17

  Tarehe: 28 May 2007 at 10:41 Anonymous Anonymous Anasema:
Simon,
naona picha zinaanza kujazana juu ya picha yako. Hongereni mliojitolea. Tuendelee kusubiri.
Afadhali zinaongezeka.Lakini bado hazitoshi.Tarehe sita si mbali.
  Tarehe: 30 May 2007 at 01:19 Anonymous Anonymous Anasema:
Safi sana Simon,
Sasa tukutane wapi unipe hela za pilau,t-shirts na sukari?
  Tarehe: 30 May 2007 at 07:30 Blogger luihamu Anasema:
Mzee Simon hongera ndugu yangu kwa kuchukuwa hatua hii ya kuwania uongozi.
@Jeff:Tukutane pale chini ya mwembe. pilau,kidogodogo, na kadhalika zinapatikana:-)
@Rasta:Asante! Na hongera kwako kwa kuwa mstari wa mbele katika maswala yote yahusuyo jumuiya hii changa.
  Tarehe: 3 June 2007 at 16:17 Anonymous Anonymous Anasema:
Heko!, kura yangu unayo braza!
Kuna tatizo moja tu!Sina upinzani mpaka sasa katika ukatibu. Kuna kitu kimoja nahisi watu hawajastuki! Hii jumuiya nauhakika itakuwa na nguvu sana ikijengwa sawa!Sasa hivi nahisi kuna watu hawaelewi hii kitu! Ukweli ni kwamba, ni maswala ya kujitolea na hakuna atakaye tajirika kifweza, lakini nahisi kunawatu hawaja stukia utajiri wa kauli na wakuwakilisha, jumuiya inavyoweza kuurutubisha.Ningefurahia sana kama watu wengi wangeendelea kujitokeza katika kujaribu kuimarisha jumuiya hii. Na naamini jumuiya hii inaweza kuwa kipaza sauti kizuri sana kwa yale yote tunayoshindwa kuyafikisha kulikoni, kutokana na ukiritimba.

Gombeeeni wadau kama unajua kuwa unaweza kuchangia kujenga jumuia hiii!
  Tarehe: 10 June 2007 at 06:27 Anonymous Anonymous Anasema:
Simon,
Nishagombea basi, mimi na wewe.
@Miriam: Ukiniuliza mimi nahisi wewe unahitajika zaidi sasa katika Jumuwata. Kura yangu unayo.
  Tarehe: 10 June 2007 at 09:36 Blogger luihamu Anasema:
Kura yangu Mkuu unayo.
Miriam na Kitururu!! nasema moto utawaka katika uchaguzi huu.
Naona Uchaguzi umekaribia. Kitu kizuri ni kwamba inamaanisha kuwa hivi karibuni maswala ya Jumuiya yatapiga hatua nyingine mbele. Kwa yeyote atakaye chaguliwa naamini atawakilisha itakiwavyo.Nafikiri maswala haya ya jumuiya na chaguzi zake haya chukuliwi kuwa nani kashinda na nani kashindwa, ila nani kachaguliwa kuwakilisha kama kiongozi na nani anawakilisha kama mwana jumuiya.

Tukiachana na hilo! Hiii bado ni swala la uchaguzi!Bloga wa picha Issa Michuzi nikikuomba uniwakilishe katika kama Mwenyekiti wa kinyang'anyiro changu , utakataa? Niwakilishe basi!
Duh!Sasa ni kweli!Kaka Issa Michuzi ndio aniendesheaye kampeni ya uchaguzi!
  Tarehe: 16 June 2007 at 09:32 Blogger Mkina Anasema:
Wa jina, unajua mambo haya bwana yana mengi, leo tena twaonana bloguni, nimechoka na kuanza kuchoshwa na matembezi ya kuwasaka wapiga kura wetu. Sijui mwenzangu watumia mbinu gani kuwapata...hebu niulize, tunaruhusiwa katakrima kidogo? Jibu tafadhali
  Tarehe: 17 June 2007 at 19:17 Anonymous Anonymous Anasema:
Simon, endapo tutakupa nafasi ya ukatibu, utawasaidiaje wana jumuiya wasio na blogu kuwa nazo.Kwani wapo wengi wahitajio wasio nazo.
Naomba jibu lenye mkakati unaoerlezeka sio siasa.
Kura yangu kwako yategemea uhawishi wa jibu lako.
Pius
  Tarehe: 22 June 2007 at 02:24 Anonymous Anonymous Anasema:
Katibu mtarajiwa mimi nataka tumtumie Jack kwenye kampeni yako,mimi nitakuwa mpiga debe namba moja wa kwako,nikisema jack nadhani unaelewa namaanisah kinywaji cha namna gani,hahahaha.umepita hauna mpinzani
Kitururu, nimelifanyia kazi ombi lako la kuongeza vitu ili wagombea waonekane katika ukurasa wa kwanza.